
JamiiForums
June 9, 2025 at 12:32 PM
SINGIDA: Mdau wa JamiiForums.com anadai Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wanaoomba uhamisho wamekuwa wakikutana na usumbufu kutoka kwa Maafisa wanaohusika kupokea taarifa kutoka Makao Makuu ya UTUMISHI au TAMISEMI
Anadai hadi Mamlaka ya juu inakubali uhamisho ni kwamba umejiridhisha na sababu zilizotolewa lakini Maafisa wa Halmashauri hiyo wanawakwaza wengi kwa kukwamisha au kuchelewesha taratibu za uhamisho
Anaeleza kuwa Serikali ilipotambulisha uhamisho wa Kidigitali walitegemea utaboresha lakini hali imekuwa ngumu, hivyo anatoa wito kwa Katibu Mkuu UTUMISHI na Katibu Mkuu TAMISEMI na Waziri wa UTUMISHI kufuatilia kero hiyo ambayo imekuwa kikwazo kwa wengi na inashusha thamani ya Utumishi wa Umma
Soma https://jamii.app/SingidaUtumishi

😢
👍
🙏
🇹🇿
📼
😂
15