
JamiiForums
June 10, 2025 at 06:57 AM
DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai Wakazi wa Mtaa wa Makamba, Mbezi Msakuzi hawana Huduma ya Maji kwa madai kuwa Mhandisi amesitisha uchimbaji mtaro "kwa sababu binafsi", Mamlaka inayohusika imetoa ufafanuzi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar (DAWASA), Everlasting Lyaro amesema walifanya vikao Machi 2025 na Ofisi ya Serikali za Mtaa wa Msakuzi Kusini na kuwaeleza hakuna fedha taslimu inayotakiwa kutolewa na Mwananchi kwa DAWASA, hivyo maunganisho mapya (Water connections fee) yatalipiwa baada ya kukamisha hatua za upimaji (Survey)
Amesema “Mtumishi wa DAWASA haruhusiwi kupita na kuchangisha fedha kwa Wananchi ili atoe huduma kwa upendeleo, Mamlaka imeweka utaratibu wa kutambulisha Watumishi wanaotekeleza miradi na wanaohudumia Wananchi.”
Soma https://jamii.app/MbeziMsakuziMaji

👍
❤️
🙏
👏
9