JamiiForums

JamiiForums

716.2K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
June 10, 2025 at 12:04 PM
TABORA: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) leo Juni 6, 2025 kimeandika kuwa Watu waliokuwa na mapanga na visu wamevamia mkutano wao maeneo ya Igunga na kufanya vurugu, ikielezwa walianza kwa kurushia mawe msafara wa Makamu Mwenyekiti wa #chadema, John Heche Taarifa hiyo imeongeza “Jeshi la Polisi halikuwepo eneo la mkutano licha ya kuwa na taarifa ya kuwepo kwa mkutano, Polisi walifika baada ya tukio hilo kutokea. Watu hao wamedhibitiwa na Wananchi.” Jitihada za kupata taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi kutoka Mkoani Tabora zinaendelea Soma https://jamii.app/MkutanoCHADEMAIgunga
👍 😢 😂 😮 🇹🇿 🙏 ❤️ 💔 💩 40

Comments