JamiiForums

JamiiForums

716.2K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
June 11, 2025 at 09:57 AM
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeendelea kusikiliza hoja za rufaa kupinga kifungo cha Maisha jela walichohukumiwa aliyekuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Clinton Damas, maarufu Nyundo na wenzake Amin Lema, Nickson Jackson na aliyekuwa Askari Magereza, Praygod Mushi, huku upande wa Jamhuri ukiomba kuzijibu Juni 12, 2025 Akiwasilisha hoja Mahakamani, Juni 10, 2025, Wakili wa Warufani hao, Godfrey Wasonga amedai kulikuwa na dosari za Kisheria katika kesi hiyo kuanzia hati ya mashtaka hadi hukumu. Amedai Mahakama ilioneshwa vipande Vinne vya Video ambavyo ni 6, 7, 8 na 9 lakini kwenye hukumu, vipande vya Video vilivyowatia hatiani ni namba 1, 2, 3 na 4 ambavyo havikuoneshwa Mahakamani hapo Aidha, kwa mujibu wa Wakili huyo, vipande vya Video vilivyooneshwa viliwaonesha washtakiwa wakijirekodi wakiwa wanacheza Muziki, huku wakiwa na chupa za Vinywaji lakini hazikuonesha wakiwa wanatenda kosa la kubaka kwa kikundi wala kulawiti Soma https://jamii.app/UpdatesKesiYaNyundo
Image from JamiiForums: Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeendelea kusikiliza hoja za rufaa kupin...
😂 😢 👍 😮 🙏 🔨 ❤️ 🇹🇿 🎃 🖕 30

Comments