
JamiiForums
June 12, 2025 at 08:28 AM
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara, John Heche amesema Mtu aliyemuomba radhi katika ‘clip’ inayosambaa ni raia ambaye alifanya hivyo kwa niaba ya Mtoto wa dada yake ambaye alifanya vurugu wakati wa Mkutano wa chama hicho
Heche amesema “Huyu bwana alionesha ustaarabu wa hali ya juu kwa kukiri kosa la mtoto wa dada yake, anachofanya RPC ni kuficha madhaifu yao na kubadili ukweli wa mambo, hakuna sehemu yoyote katika mazungumzo hayo mtu huyo amejitambulisha kuwa ni Askari.”
Ikumbukwe, Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Abwao aliwaambia Wanahabari kuwa wamemkamata mtu huyo Daud Paul Delim (49), Mkazi wa Mbagala A, Wilayani Igunga ikielezwa alijifanya ni Mkuu wa Kituo cha Polisi
Soma https://jamii.app/HecheMkoaniTabora

👍
😂
🙏
❤️
📌
😢
25