JamiiForums

JamiiForums

716.2K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
June 12, 2025 at 01:19 PM
KENYA: Mamia ya Waandamanaji wamekusanyika katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi na Miji mingine wakitaka haki itendeke kwa maafisa waliohusika na kifo cha Mwanamitandao Albert Ojwang', pamoja na kupinga mipango ya Serikali kuhusu Bajeti mpya inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni rasmi leo Juni 12, 2025 jioni na Waziri wa Fedha, John Mbadi Kumekuwa na taarifa kwamba Serikali inapanga kusoma Bajeti mpya bila kubadilisha hatua kali za kodi kama vile kuongeza ada za huduma muhimu au kupunguza kodi kwa bidhaa za msingi kama mafuta na chakula, ambazo zilisababisha #maandamano makubwa ya Juni 2024 yaliyosababisha vifo, majeruhi, na uharibifu mkubwa wa mali Hata hivyo, waandamanaji wameeleza hofu yao kuwa huenda Serikali ikatumia mbinu zilezile, wakisisitiza umuhimu wa #uwazi na ushirikishwaji kamili katika maamuzi yote ya kifedha yanayowahusu moja kwa moja Soma https://jamii.app/MaandamanoBajeti25
Image from JamiiForums: KENYA: Mamia ya Waandamanaji wamekusanyika katika maeneo mbalimbali ji...
😂 👍 ❤️ 👏 💯 😮 🙏 🫶 12

Comments