Bank of Tanzania

Bank of Tanzania

296.6K subscribers

Verified Channel
Bank of Tanzania
Bank of Tanzania
May 14, 2025 at 07:49 AM
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Emily Burns, katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam, tarehe 13 Mei 2025. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali yahusuyo biashara na uwekezaji, ambapo Gavana Tutuba alieleza kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji, hatua ambayo imekuwa chachu ya ukuaji wa uchumi pamoja na kuvutia wawekezaji wa ndani na wa nje kuwekeza katika sekta mbalimbali. Kwa upande wake, Balozi Burns alitoa pongezi kwa Benki Kuu kwa jitihada inazoendelea kuzifanya katika kuimarisha uchumi wa taifa. Aidha, aliahidi kuwa Serikali ya Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya pande zote mbili. https://www.instagram.com/p/DJmzgG8OWIA/?igsh=bTNmbmtndm5uNTMw
🙏 👍 ❤️ 😢 😂 😮 🇨🇦 😇 49

Comments