
TCRA TANZANIA
May 14, 2025 at 04:18 AM
TCRA imeshiriki katika mkutano uliowaleta pamoja Watoa Huduma za Utangazaji (CSPs) na TCRA kujadiliana kuhusu Utangazaji wa Kidijiti wa Redio sambamba na kikao cha mashauriano kuhusu uanuai wa maudhui ya utangazaji katika Ukumbi wa Mikutano wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, tarehe 12 Mei 2025.
Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni Watoa Huduma za Utangazaji wa Redio kutoka mikoa ya Njombe, Katavi, Songwe, Mbeya na Iringa kwa lengo la kuwaongeza uelewa wa watoa huduma kuhusu ujio wa Teknolojia ya Utangazaji wa Redio kidijiti (DSB), pamoja na kufanya mashauriano kuhusu hatua za kuongeza uanuai wa maudhui ya utangazaji yanayoakisi jamii zote, yanayoangazia sekta mtambuka za uchumi na jamii na kukuza maudhui ya ndani.
Watoa huduma walipata uelewa kuhusu utangazaji wa kidijiti na kubaisha utayari wao kupokea ujio wa DSB utakaoboresha utangazaji zaidi.
#tcratz #digitalsoundbroadcasting #elimukwaumma

👍
3