TCRA TANZANIA

TCRA TANZANIA

256.0K subscribers

Verified Channel
TCRA TANZANIA
TCRA TANZANIA
May 19, 2025 at 05:09 PM
📌TCRA YATOA ELIMU YA USALAMA MTANDAONI KWA MASHEHA 36, PEMBA 📍WETE - PEMBA 🗓️ 19/05/2025 Ofisi ya TCRA Zanzibar ikiongozwa na Meneja Bi. Esuvatie - Aisa Masinga imeandaa na kuratibu Semina ya Matumizi Salama ya Mtandao kwa Masheha 36 wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za "NI RAHISI SANA" na “SITAPELIKI” zinazohamasisha usalama mtandaoni kwa kila mtumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano. Semina hii imetoa fursa kwa Masheha kuelezea majaribio ya utapeli waliyowahi kukutana nayo, pamoja na kupewa elimu ya jinsi ya kutambua, kuripoti na kujiepusha na utapeli mtandaoni. Kupitia semina hii, TCRA imewahimiza Masheha kutoa elimu kwa wananchi wa shehia zao kuhusu vidokezo vya usalama mtandaoni, kama vile matumizi ya nywila thabiti, kutofuata maelekezo ya kutuma pesa au kutoa taarifa binafsi kwa watu wasiowafahamu mitandaoni, kuepuka kubofya viunganishi bila kujua usalama wake, kuhakiki namba zilizosajiliwa kwa vitambulisho vyao vya Taifa kupitia *106#, kuwasiliana na watoa huduma kupitia namba 100 pamoja na kuripoti majaribio ya utapeli kupitia namba 15040. #tcratz #elimukwaummama #uchumiwakidijiti #klabuzakidijiti #nirahisisanakuwasalamamtandaoni #nirahisisana #sitapeliki #usalamamtandaoni
👍 🙏 😢 10

Comments