
TCRA TANZANIA
May 29, 2025 at 10:17 AM
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshiriki kwenye kikao-kazi na wadau wa Shirika la Usimamizi wa Mawasiliano kwenye Mtandao wa Intaneti (ICANN), kilichofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Mei, 2025. Kikao hicho kimefunguliwa rasmi na mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA kutoka TCRA, Bi. Tusajigwe Mwalukasa kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Ajenda kuu ya kikao hiki ilikuwa kutoa uelewa kwa wadau kuhusu awamu ijayo ya majina mapya ya viwango vya juu vya vikoa - New Generic Top-Level Domains (New gTLDs).
Kupitia kikao hiki, shirika la ICANN limetambulisha programu ya kujengea uwezo wadau wanaostahiki, ili kukamilisha mchakato wa uombaji wa majina mapya ya vikoa (domain) yanayosaidia kuongeza wigo wa majina yanayotumika kwenye mtandao wa intaneti na kulinda chapa zao mtandaoni. TCRA inawaalika wadau na taasisi zinazotaka kufanya mchakato wa maombi ya majina haya kuwasiliana nasi kupitia dawati la huduma kwa wateja kwa namba 0800008272 au baruapepe: [email protected] ili kupata mwongozo wa mc
👍
😂
🙏
3