
TCRA TANZANIA
May 30, 2025 at 05:14 AM
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hutoa ripoti za Takwimu za Sekta ya Mawasiliano kila robo ya mwaka wa fedha, kwa lengo mahsusi la kutoa taarifa za mwenendo wa sekta ya mawasiliano kwa sekta ndogo za Posta, Utangazaji pamoja na Simu na Intaneti. Ripoti hizi pia ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya TCRA kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) namba 12 ya mwaka 2003.
Ripoti za Takwimu za Mawasiliano zinapatikana kwenye tovuti ya TCRA kupitia www.tcra.go.tz, sehemu ya machapisho kisha kipengele cha Takwimu za Mawasiliano au kupitia kiunganishi hiki https://www.tcra.go.tz/services/statistics
#tcratz #statistics #tanzania #stakeholders #sektayamawasiliano #posta #simunaintaneti #utangazaji
👍
🙏
3