TCRA TANZANIA

TCRA TANZANIA

256.0K subscribers

Verified Channel
TCRA TANZANIA
TCRA TANZANIA
June 10, 2025 at 04:44 PM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekabidhi tuzo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuwa miongoni mwa Taasisi zilizochangia kiasi stahiki na kwa wakati, kwa mfululizo wa miaka mitano, kuanzia mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2024/25. Tuzo hiyo imepokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TCRA Dkt. Jones Killimbe, pamoja na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Jabiri Bakari, katika hafla ya kupokea Gawio na Michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma (Gawio Day 2025), tarehe 10 Juni 2025, Ikulu Dar es Salaam. TCRA imeongoza katika kundi la Taasisi zilizochangia wastani wa bilioni 27.5 ndani ya miaka mitano mfululizo, ikifuatiwa na TASAC (bilioni 21.7) pamoja na BRELA (bilioni 15.8). #gawio2025 #tcratz 📷 https://www.instagram.com/p/DKujTcfuk3d/?img_index=1
Image from TCRA TANZANIA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu H...
👍 3

Comments