
TCRA TANZANIA
June 11, 2025 at 12:35 PM
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini Mhandisi Francis Mihayo pamoja na Afisa Mawasiliano wa TCRA Bi. Herieth Shija wakitoa elimu kwa umma kuhusu kampeni ya Ni Rahisi Sana Sitapeliki walipotembelea katika kituo cha redio cha Zion Impact kilichopo jijini Arusha.
Kwenye mahojiano jamii imehimizwa kutumia nywila thabiti kujilinda wanapokuwa wanatumia huduma za mawasiliano hasa ya simu na intaneti.
Pia wananchi wametakiwa kuendelea kuripoti utapeli kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 15040, kuhakiki laini ya simu kwa namba *106# na kuwasiiana na mtoa huduma kupitia namba 100 pekee.
#tcratz #nirahisisana #sitapeliki #elimukwaumma #klabuzakidijiti #digitalclubs

❤️
👍
4