
Dr. BUDODI
May 16, 2025 at 10:39 AM
Ilikuwa majira ya jioni nikiwa ofisini ndipo nilipokea simu kutoka kwa mwanamke ambaye tangu mwanzo wa maongezi alikuwa na sauti ya woga na majuto. Alikuwa Mama Aisha, mwanamke mwenye umri wa miaka 28, ambaye alikuwa amepata huduma za Post-Abortion Care (PAC) wiki nne zilizopita baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba. Sauti yake ilikuwa imejaa hofu: "Daktari, nimeanza kuhisi kichefuchefu tena… je, inawezekana niko na mimba nyingine?" aliuliza kwa hofu. Kwa kipindi chote cha udaktari wangu, nimepokea simu kama hizi nyingi. Leo, nataka ujifunze kupitia kisa hiki.
