
Dr. BUDODI
90 subscribers
About Dr. BUDODI
Afya karibu yako. Dondoo za Afya Elimu na Vifaa tiba. afya bora ndio msingi wa furaha Maishani
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

*UTE HUHUSIKA VIPI KWENYE UJAA UZITO?* Mlango wa kizazi hutengeneza ute(cervical Mucus) kwaajili ya kulinda kizazi lakini pia kwaajili ya kusaidia mbegu za mwanaume kusafiri kwenda kwenye yai na kutungisha mimba. Ute huu ukiwa mzito zaidi ya kawaida, ukiwa na hali ya asidi, au ukiwa na seli za kinga ya mwili ambazo hushambulia mbegu za kiume ute huathiri uwezo wa mbegu kusafiri na hata kuzishambulia na kuziua kabla hazijaingia kwenye kizazi. Mwanamke anaweza kuwa na hali hii sababu ya changamoto za homoni (mf, viwango vya chini vya estrogen au viwango vya juu vya Progesterone), maambukizi kwenye kizazi, matumizi ya dawa kama clomiphene, au magonjwa kama polycystic ovarian syndrome (PCOs). Ute usiofaa hupunguza uwezo wa mbegu kuishi hadi chini ya saa moja badala ya siku 3-5. Dalili zinaweza kujumuisha ukavu ukeni, maumivu wakati wa tendo au hedhi zisizo za kawaida. Mara nyingi hugunduliwa kwa kipimo cha ute baada ya tendo(postcoital test). Kwa upande mwingine kujifunga kwa mlango wa kizazi(Cervical Stenosis), hutokea wakati njia ya mlango wa kizazi inapokuwa nyembamba sana au kujifunga kabisa kutokana na makovu ya upasuaji au vipimo vya kutoa nyama kwenye Cervix (mf. LEEP au cone biopsy). Maambukizi ya mara kwa mara, au matibabu ya mionzi baada ya kuugua kansa ya mlango wa kizazi pia husababisha. Mambo haya huzuia mbegu za kiume kuingia au ute kufanya kazi vizuri, na kuongeza utengenezwaji wa ute usiofaa. Dalili zinaweza kujumuisha maumivu makali wakati wa hedhi au kupata damu kidogo, lakini mara nyingi hazionekani hadi utakapofanyiwa vipimo. *INASABABISHAJE UTASA?* Ute usiofaa unazuia mbegu za kiume kufika kwenye yai kwa kuziua au kuzifanya zipoteze nguvu, ikifanya urutubishwaji wa yai kwa njia za kawaida kuwa mgumu. Hata kama mbegu chache zinafika, hatari ya kuharibika kwa mimba huongezeka kwa ~10-15% kutokana na mazingira yasiyo rafiki. Kujifunga kwa mlango wa kizazi huongeza tatizo kwa kuzuia mbegu za kiume kuingia kabisa au kuharibu ubora wa ute, ikipunguza nafasi za ujauzito na kupunguza ufanisi wa njia za upandikizaji kwa ~5-10%. *NJIA SALAAMA NA SAHIHI YA KUPATA MTOTO.* Njia za upandikizaji husaidia wanawake wenye changamoto hizi kupata watoto. * _Intrauterine Insemination (IUI):_ Kwa njia hii mbegu za kiume huwekwa moja kwa moja kwenye mji wa mimba au mirija ya uzazi kipindi cha ovulation, ikiepuka changamoto ya ute usiofaa na mlango wa kizazi uliojifunga. * _Cervical Dilation:_ Njia hii ya upasuaji inafungua mlango wa kizazi uliojifunga na kuruhusu IUI au IVF kufanyika kwa ufanisi mkubwa. * _In Vitro Fertilization (IVF):_ kwa njia hii mayai huvunwa kutoka kwa mwanamke kipindi cha ovulation na kuyarutubisha kwenye maabara, na mtoto aliepatikana hupandikizwa kwenye kizazi. Njia hii huepuka changamoto zote za mlango wa kizazi na hata zile za mirija ya uzazi. *USHAURI WA KITAALAMU.* Ikiwa una uke mkavu, hedhi zisizo eleweka, au historia ya upasuaji wa mlango wa kizazi, wasiliana na daktari mapema ambapo atapendekeza kipimo cha ute baada ya tendo (postcoital test) na hysteroscopy ili kugundua ute usiofaa na mlango wa kizazi kujifunga. IUI ni njia nzuri zaidi kwa wagonjwa wa tatizo hili, na cervical dilation inaweza kusaidia ikiwa mlango wa kizazi umejifunga. Usichelewe, kwani umri zaidi ya miaka 35 hupunguza ufanisi wa njia za upandikizaji. Jikinge na maambukizi ya mara kwa mara kwenye kizazi kwa kufanya ngono salama na kupata matibabu haraka ukiugua pia epuka matumizi ya hovyo ya clomiphene. Daktari atakupa msaada wa kisaikolojia utakaokusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo kipindi cha matibabu. Kula chakula chenye vitamini E kwa wingi na kunywa maji mengi ili kuboresha afya ya ute wako. Kwa kuzingatia haya utaitwa mama.

KUGAWANYIKA KWA KIZAZI HUSABABISHA UTASA Changamoto za kimaumbile mbali mbali zinazotekea ndani ya mji wa mimba husababisha utasa. Kugawanyika kwa kizazi(Bicornuate/ Septate Uterus) inaathiri ~2-5% ya wanawake wenye utasa.Hali hii hufanya iwe vigumu kwa wanawake hawa kupata mimba bila matibabu. *KUGAWANYIKA KWA KIZAZI NI NINI?* Mji wa mimba huota nyama(tishu) ambayo huugawanya katika sehemu mbili tofauti(Septate Uterus)na katika hali nyingine, mji wa mimba hugawanyika kuanzia nje na kutengeneza pande mbili tofauti. Hali hizi ni za kuzaliwa nazo(congenital anomalies) huathiri moja kwa moja utendaji kazi wa mji wa mimba kama kuweza kuhifadhi mimba na hata kuruhusu mbegu na yai kukutana. Hali hizi zinaweza rithishwa kati ya wanafamilia lakini matumizi ya kemikali kama diethylstilbestrol (DES) wakati wa ujauzito huongeza hatari ya changamoto hizi. Dalili zinaweza kujumuisha kuharibika kwa mimba mara kwa mara, hedhi zenye maumivu makali, maumivu ya nyonga, lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili hadi pale wanaposhindwa kupata ujauzito. Kasoro hizi za kimaumbile hugunduliwa kwa ultrasound, MRI, au hysteroscopy. *INASABABISHAJE UTASA?* Mgawanyiko wa kizazi hutengeneza mazingira magumu kwa mimba kutunga na pia huathiri ubora wa kuta za mji wa mimba kwa kupunguza mzunguko wa damu kwenye kizazi. Mimba hupandikizwa kwenye kuta zisizo na ubora hali ambayo huongeza hatari ya kuharibika kwa mimba kwa ~30-50% pia inasababisha mwanamke kujifungua kabla ya muda kwa. *NJIA SALAMA ZA KUBEBA UJAAUZITO.* * _Hysteroscopic Septum Resection(upasuaji):_ Njia hii ya upasuaji husaidia kurekebisha maumbile yasiyo sahihi. Inaweza tumika pekeake ambapo mwanamke ataweza kubeba mimba kwa njia za kawaida au inaweza tumika kabla ya IVF ili kuongeza ufanisi wa njia hizi za upandikizaji * _In Vitro Fertilization (IVF):_ Baada ya upasuaji njia hii ya upandikizaji hutumika kuhakikisha mwanamke huyu anabeba mimba. Mayai huvunwa kutoka kwa mwanamke na urutubishaji utafanyika maabara na watoto watakaopatikana hupandikizwa kwenye kuta za mji wa mimba na mwanamke huyu hubeba ujaauzito. *USHAURI WA KITAALAMU* Ikiwa una historia ya kuharibika kwa mimba mara kwa mara, hedhi zenye maumivu makali, au unashindwa kupata ujauzito kabisa. wasiliana na daktari ambapo atapendekeza vipimo kama ultrasound, MRI, au hysteroscopy ili kugundua kasoro za kizazi kugawanyika. Hysteroscopic resection ni hatua ya kwanza katika kutibu Septate Uterus, na inaweza kurejesha uwezo wa mwanamke kubeba mimba kawaida au kuboresha IVF. Usichelewe, kwani umri zaidi ya 35 hupunguza ufanisi wa njia za upandikizaji. Epuka dawa au kemikali zinazoweza kuathiri homoni zako. Daktari atakupa ushauri wa kisaikolojia utakaokusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo kipindi cha matibabu, hasa ikiwa mimba zimeharibika mara kadhaa. Kula chakula chenye vitamini D na omega-3 ili kuimarisha afya ya mji wa mimba. Zingatia haya kwa usahihi na utaitwa mama!.

Changamoto za kimaumbile mbali mbali zinazotekea ndani ya mji wa mimba husababisha utasa. Kugawanyika kwa kizazi(Bicornuate/ Septate Uterus) inaathiri ~2-5% ya wanawake wenye utasa.Hali hii hufanya iwe vigumu kwa wanawake hawa kupata mimba bila matibabu.


Mlango wa kizazi(Cervix) hulindwa na ute ambao husaidia mbegi za kiume kusafiri kiurahisi kipindi cha ovulation kuelekea kwenye mji wa mimba. Ikitokea ute huu hauna sifa zinazosaidia mbegu kisafiri na pengine hata kuzidhuru mbegu basi inakua vigumu kwa mwanamke kubeba mimba. Ute usiofaa kwenye mlango wakizazi, unaathiri 5-10% ya wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito, huku kujifunga kwa mlango wa uzazi(Cervical Stenosis) ikichangia kwa ~3-5%. Magonjwa haya hufanya iwe vigumu kwa mwanamke kuzaa..Bila matumizi ya njia za kisasa za upandikizaji ni vigumu kwa wanawake hawa kupata mimba kwa njia za kawaida.
