Dr. BUDODI
Dr. BUDODI
June 5, 2025 at 03:30 PM
*Inatokeaje?* Hyperprolactinemia hutokea wakati mwili wako unatoa homoni ya prolactin kwa wingi, homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa. Prolactin hutolewa na tezi ya pituitari kwenye ubongo, lakini ikizidi, inazuia homoni nyingine inayoitwa GnRH, ambayo inaamuru ovari kutoa homoni za FSH na LH zinazohitajika kwa ukuaji wa yai. Sababu za kawaida ni pamoja na uvimbe mdogo kwenye tezi ya pituitari (microadenoma), matumizi ya aina fulani ya dawa kama dawa za magonjwa ya akili (antipsychotics), au hali kama hypothyroidism (tezi ya thyroid isiyofanya kazi vizuri). Dalili zinaweza kujumuisha maziwa kuvuja(galactorrhea), hedhi zisizo eleweka au kukosa hedhi kabisa, maumivu ya kichwa, au matatizo ya kuona ikiwa uvimbe ni mkubwa. Hali hii mara nyingi hugunduliwa katika miaka ya 20 hadi 30, lakini inaweza kutokea wakati wowote. *Inasababishaje ugumba?* Hyperprolactinaemia inazuia GnRH, ikisababisha ovari kushindwa kutoa yai kwa sababu homoni za FSH na LH hazitolewi vya kutosha. Bila ovulation, hakuna yai linalopatikana kwa mbegu za kiume kuungana nalo, na hivyo kufanya iwe vigumu kupata ujaauzito. Hata kama ovulation itatokea mara kwa mara, hedhi zisizo za kawaida hupunguza nafasi za kupata ujauzito, na mivurugiko ya homoni huongeza hatari ya mimba kuharibika kwa ~10-20%. *Njia salama na sahihi ya kupata ujaauzito lwa mgonjwa wa Hypoproteinemia.* Matibabu ya kisasa yanatoa suluhisho. * _Matibabu ya Dawa pamoja na Intrauterine Insemination (IUI):_ hutumia dawa kama dopamine agonists (mfano, cabergoline) kupunguza prolactin na kurejesha ovulation, ikifuatwa na IUI ambapo mbegu za kiume zinawekwa kwenye mirija ya uzazi. * _In Vitro Fertilization (IVF):_ hutumiwa ikiwa dawa hazifai, ikichukua mayai na kuyarutubisha kwenye maabara. *Ushauri wa Kitaalamu.* Ukipata dalili kama maziwa kuvuja, hedhi zisizo za kawaida, au maumivu ya kichwa, na ikiwa unashindwa kupata ujauzito ama kila mimba unazobeba zinaharibika. Wasiliana na daktari kwa vipimo vya prolactin na picha za tezi ya pituitari (kama MRI). Daktari anaweza tumia dawa ambazo mara nyingi hurejesha ovulation ndani ya miezi michache. Ikiwa ovulation itarejea na hakuna shida nyingine basi utaweza kuzaa. Ikishindikana mtaalamu wa afya atakuanzishia program ua IUI kabla ya kuendelea na IVF. Anza mapema, kwani umri zaidi ya 35 unaathiri matokeo. Dhibitu uzito wako (BMI 18.5-24.9) na epuka dawa zinazoongeza prolactin, kama baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili. Daktari atakupa ushauri wa kisaikolojia utakaokusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo kipindi cha matibabu. Kwa kuzingatia kliniki na maelekezo ya daktari utapata mtoto.
🙏 1

Comments