Dr. BUDODI
Dr. BUDODI
June 6, 2025 at 07:18 PM
*Endometriosis inasababishaje utasa?* Endometriosis ni hali ambapo tishu zinazofanana na za ndani ya mji wa mimba(endometrium) huota nje ya uterasi, mara nyingi kwenye ovari, mirija ya uzazi, au sehemu za nyonga. Tishu hizi huzingatia mihemko ya homoni za hedhi kama kuvuja damu kila mwezi, na hivyo zikiwa sehemu isiyostahili husababisha michubuko na kuvimba, makovu, au uvimbe maji kwenye ovari (ovarian Cyst). Makovu haya yanaweza kuziba mirija ya mayai au kuiharibu, yakizuia yai na mbegu za kiume kukutana au kijusi kusafiri hadi kwenye mji wa mimba(uteras). Michubuko na uvimbe huharibu ubora wa mayai na mazingira ya uterasi hivo hupunguza uwezekano wa mimba kutunga, na kuongeza hatari ya kuharibika kwa mimba kwa ~20-40%. Mirija iliyoziba pia inaweza kusababisha mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy), ambapo mimba hutunga kwenye mirija ya uzazi. hali inayohitaji matibabu ya haraka.Hakuna Sababu za moja kwa moja za endometriosis, lakini wataalamu wanaamini inaweza kutokana na damu ya hedhi kurudi nyuma (retrograde menstruation) ambayo inaweza tokea ikiwa unafanya mapenzi wa kati wa hedhi, kurithi, au mabadiliko ya homoni. Hali hii mara nyingi hutokea kwa wanawake wa miaka 20 hadi 40, na inaweza kuwa ya wastani(Hatua I-II) au kali (Hatua III-IV), ambapo makovu mengi yanaziba mirija. *Njia salama na sahaihi ya kumsaidia mwanamke mwenye Endometriosis.* Njia za upandikizaji husaidia kwa kiwango kikubwa * _In Vitro Fertilization (IVF):_ Yai lenye ubora litachukuliwa kutoka kwa mwanamke na urutubishaji utafanyika maabara. Baada ya urutubishaji mtoto aliepatikana hupandikizwa kwenye kizazi cha mwanamke husika. Njia hii husaidia kuepuka changamoto zote za mirija. * _Upasuaji(Laparoscopic Surgery):_ Oparesheni hii huondoa tishu za endometriosis ili kuruhusu mwanamke aweze kuzaa kawaida au kuboresha IVF. * _Intrauterine Insemination (IUI):_ Njia hii hutumika ikiwa endometriosis haijafikia hatua za mwisho ikijumuishwa na dawa ufanisi huwa mkubwa zaidi. *USHAURI WA KITAALAMU.* Ikiwa una hedhi zenye maumivu makali, au unashindwa kupata ujauzito, ni vema ukawahi kupata msaada wa afya ambapo vipimo kama ultrasound au laparoscopy vitafanyika ili kugundua endometriosis. Kuwahi kuanza matibabu ni muhimu, kwani makovu yanaweza kuwa na madhara zaidi kadili muda unavozidi kwenda. Upasuaji unaweza kusaidia kwa hatua za mwanzo, lakini IVF ni bora kwa endometriosis ilio katika hatua za mwisho. Daktari atafanya vipimo vya AMH ili kuangalia ubora wa mayai yako, na nivema kuanza matibabu kabla ya umri wa miaka35, kwani umri unaathiri sana matokeo ya matibabu. Wakati wa matibabu Daktari atakupa dawa za kupooza maumivu na atapendekeza Kula chakula bora chenye virutubisho kama omega-3(mafuta ya samaki) ili kupunguza michubuko na uvimbe. Usitibu chango kwa kutumia dawa za maumivu tuu fika hospital kwa vipimo zaidi. ---

Comments