
Dr. BUDODI
June 8, 2025 at 12:57 PM
Tofauti na kuwa mirija ya uzazi(fallopian tubes) hutengeneza muumganiko wa moja kwa moja kati ya mayai yako na mji wa mimba(Uterus) lakini mirija hii hutumika kama sehemu ya urutubishaji wa yai. Hivo ikitokea mirija imeziba kwa sababu yeyote ile ni vigumu kwa mwanamke kuneba mimba. Ugonjwa wa PID(Maambukizi ya bacteria kwenye kizazi) unachangia kwa zaidi ya 60% kwa wanawake kupata utasa, na hufanya hivyo kwa kuathiri mirija na hata kuiziba kabisa. PID huwa na dalili kama kutokwa na uchafu sehemu za siri ambao maranyingi huwa na harufu, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na maumivu wakati wa tendo au wakati wa haya ndogo. Dalili kama kuhisi kucheza kwa tumbo chini ya kitovu mithili ya mtoto huashiria madhara ya moja kwa moja kwenye mirija ya uzazi na mayai. Ambapo mayai hutengeneza uvimbe maji(ovarian cyst) na mirija kujaa maji (Hydrosalpinx).
