
Dr. BUDODI
June 9, 2025 at 03:09 PM
*UPASUAJI UNAHUSIANA VIPI NA UTASA?*
Mirija ya uzazi( fallopian tubes) huunganisha mji wa mimba na mayai. Ikitokea kwa makusudi au bahati mbaya mirija imekatwa mawasiliano haya huvunjika na kuathiri utendaji kazi wa mfumo wote wa uzazi. Changamoto kama Appendicitis ambazo hupelekea upasuaji karibu zaidi au ndani ya mfumo wa uzazi (appendectomy), uvimbe maji kwenye mayai(Ovarian Cyst), au mimba zilizotunga nje ya kizazi(Ectopic pregnancy), inaweza kuacha makovu na michubuko kwenye mfumo wa uzazi. Makovu haya yanaweza kuziba mirija ya uzazi au hata kupunguza upana wa njia, na kufanya iwe vigumu kwa yai na mbegu za kiume kukutana. Upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye kizazi kama fibroids, mayoma au polyps pia unaweza kusababisha tatizo hili. Dalili zinaweza kujumuisha maumivu ya nyonga mara kwa mara, lakini mara nyingi dalili kubwa ni kushindwa kupata ujauzito. Hali hii hugunduliwa kwa wanawake wenye umri wa kuzaa, hasa waliopitia upasuaji.
*INASABABISHAJE UTASA?*
Mirija ya uzazi iliyoziba au kuharibika kutokana na makovu ya upasuaji inazuia mbegu za kiume kufika kwenye yai, ikifanya urutubishaji wa yai kushindikana. Hata kama moja ya mirija iko wazi, makovu yanaweza kusababisha mimba kutunga kwenye mirija(ectopic pregnancy), hali hatari inayohitaji matibabu ya haraka. Michubuko kwenye kizazi kutokana na makovu pia unaweza kuharibu ubora wa yai au mazingira ya mji wa mimba, ikipunguza uwezekano wa kupata ujauzito kwa njia za kawaida na pia huongeza hatari ya mimba kuharibika kwa ~10-20%.
*ZIPI NI NJIA SALAMA ZA KUBEBA UJAAUZITO?*
* _In Vitro Fertilization (IVF):_ Njia hii huchukua mayai moja kwa moja kutoka kwenye ovari huyarutubisha kwenye maabara, na kupandikiza mtoto kwenye mji wa mimba, njia hii huepuka changamoto ya mirija
*USHAURI WA KITAALAMU*
Ikiwa una historia ya upasuaji kwenye nyonga mf.appendectomy, mimba za nje ya kizazi(Ectopic pregnancy), au uvimbe kwenye kizazi, wahi hospital ambapo Daktari atapendekeza kipimo cha Hysterosalpingography (HSG) ili kuangalia hali ya mirija yako ya uzazi. IVF ni njia bora kwa mwanamke mwenye changamoto ya mirija kuziba. Usichelewe, kwani umri zaidi ya miaka 35 hupunguza ufanisi wa IVF. Baada ya upasuaji zingatia haya ili kuepuka mirija luziba, zingatia matumizi ya dawa za kuzuia maambukizi baada ya upasuaji ili kuepuka mirija kuziba. Kula chakula bora chenye vitamini E na C ili kuimarisha kinga ya mwili na kusaidia vidonda vya upasuaji kupona vizuri . Ni muhimu kufanya vipimo vya mbegu za mume wako ili kuhakikisha ubora wake. Daktari atatoa ushauri wa kisaikolojia utakaokusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo wakati wa matibabu.