Dr. BUDODI
Dr. BUDODI
June 10, 2025 at 08:00 PM
*UVIMBE HUFANYA NINI HASA?* Kuna aina tofauti za uvumbe,kuna zinazoweza kuwa za kansa na zingime ambazo si za kansa. Uvimbe kama fibroids na Endometrial polyp au hata Mayoma hizi hazihusiani na kansa lakini zinaharibu ufanisi wa kizazi na kuzuia mimba. Kansa ya kizazi pia hisababisha kuota kwa tishu zinazozuia mimba kutunga. Uvimbe unaweza kutokea katika saizi tofauti tofauti unaweza kuwa mdogo au mkubwa, na zinaweza kukua ndani ya ukuta wa mji wa mimba (intramural), chini ya tishu za ndani (submucosal), au nje (subserosal). Aina za uvimbe zinazoota ndani ya mji wa mimba huathiri moja kwa moja utungaji wa mimba.Uvimbe ukitokea sehemu zingine kama katikati ya misuli au nje na ukiwa na saizi kuba pia huathiri utungaji wa mimba. Uvimbe hubadilisha umbo la kizazi na kufanya iwe vigumu kwa mimba kutunga ma hivyo kusababisha utasa. Sababu za uvimbe ni pamoja na kurithi kutoka kwenye familia, unene (BMI zaidi ya 30), au mvurugiko wa homoni, hasa kwa wanawake wa miaka 30 hadi 40. Dalili zinaweza kujumuisha hedhi zenye maumivu makali na kutoka damu nyingi, maumivu ya nyonga, lakini baadhi ya wanawake hawaonyeshi dalili hadi pale wanaposhindwa kupata ujauzito. Uvimbe hutambulika kwa ultrasound, MRI, au hysteroscopy. *JINSI UVIMBE UNAVYOSABABISHA UTASA* Uvimbe kwenye kizazi, hasa zile za submucosal, huzuia mimba kugunga kwenye ukuta wa mji wa mimba kwa kubadilisha umbo lake au kupunguza mzunguko wa damu kwenye tishu za ndani (endometrium), swala ambalo ni muhimu kipindi cha ujauzito. Uvimbe unaweza pia kuzuia mbegu za kiume kufika kwenye yai ikiwa ziko karibu na mirija ya uzazi. Vimbe zenye saizi kubwa (zaidi ya 3 cm) au zaidi huongeza hatari ya kuharibika kwa mimba kwa ~20-30% na hupunguza nafasi ya mwanamke kubeba mimba kwa njia za kawaida. *NJIA NZURI NA SALAAM ZA KUBEBA UJAAUZITO* Matibabu na ufanisi wa njia za kimatibabu hutegemea sana aina na ukubwa wa uvimbe * _Dawa :_ Hii hutumika kwa uvimbe aina ya fibroid zenye ukubwa mdogo ~1-3cm. Ikizingatiwa vizuri ufanisi ni mkubwa * _Hysteroscopic Surgery(Upasuaji):_ Upasuaji huu wa kisasa huondoa vimbe za ndani ya mji wa mimba kwa kutumia vifaa vyembamba ambavyo hupitia kwenye mlango wa kizazi, mgonjwa hatopata kovu wala kidonda sehemu ya tumbo. Hii hutumika kwenye Fibroid, mayoma na Polyps * _In Vitro Fertilization (IVF):_ inaweza kutumika baada ya upasuaji au kwa fibroid ambazo hazijathiri sana mji wa mimba, ikichukua mayai, kuyarutubisha kwenye maabara, na kupandikiza mtoto kwenye mji wa mimba. Ikiwa mji wa mimba umeathirika Sana basi Surrogate mother(Mwanamke wa kujitolea) anaweza tumika kumsaidia mwanamke huyu kubeba hii mimba *USHAURI WA KITAALAMU* Ikiwa una hedhi zenye maumivu makali, unatoka damu nyingi ukiwa hedhi, au unahisi kubanwa kwenye kibofu cha mkojo. Basi wasiliana mapema na daktari ambapo utafanyiwa vipimo kama ultrasound au hysteroscopy ili kugundua uvimbe. Upasuaji wa hysteroscopy ni hatua ya kwanza kwa ubombe unaoathiri mji wa mimba, na inaongeza ufanisi wa kuzaa kawaida au IVF. Usichelewe, kwani umri zaidi ya 35 hupunguza ufanisi wa matibabu. Punguza uzito ikiwa una BMI zaidi ya 30, kwani unene unachochea ukuaji wa uvimbe. Ushauri wa kisaikolojia utakusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo wakati wa matibabu. Kula chakula chenye wanga kidogo na vitamini D ili kuimarisha homoni zako.

Comments