IslamicForum
IslamicForum
May 15, 2025 at 05:22 PM
π—œπ—§π—”π—žπ—¨π— π—•π—¨π—žπ—ͺ𝗔 π—žπ—¨π—ͺπ—”πŸ‘‡ √ Pakistan lilikuwa ni Taifa lenye nguvu za nyuklia, lakini halikuweza kutoa msaada kwa Palestina hata kwa uchache wa risasi tu. √ Misri ilikuwa na mto Nile, lakini Wapalestina wa Gaza hususan watoto wadogo walikufa kwa Kiu kikali. √ Saudi Arabia na UAE walikuwa na bahari za mafuta, lakini hospitali za Gaza na gari za wagonjwa (Ambulances) hazikuwa na mafuta ya kuendeshea. √ Itakuja kukumbukwa kuwa, Mataifa ya Kiislamu yalikuwa na zaidi ya Wanajeshi milioni 5, mizinga mizito, makombora ya masafa marefu, na ndege za kivita, lakini hakuna hata kimojawapo kilichoweza kufika Gaza na kutoa msaada. Hata kama Palestina leo itakuwa huru na Taifa la Israel kufutika katika ramani, Kizazi kijacho hakitashangazwa na mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Israel kwa Wapalestina, bali kitashangazwa na ukimya wa kutochukua hatua wa Mataifa ya Kiislamu ilhali uwezo huo walikuwa wanao. ___ By: Rmunga Credit: Moaz Majeed
Image from IslamicForum: π—œπ—§π—”π—žπ—¨π— π—•π—¨π—žπ—ͺ𝗔 π—žπ—¨π—ͺπ—”πŸ‘‡  √ Pakistan lilikuwa ni Taifa lenye ...

Comments