
IslamicForum
May 16, 2025 at 09:05 AM
Na historia iandike:
Kwamba Trump aliingia katika kisiwa cha Waarabu "Jaziratul Arab", akakikuta hakina wanaume…
kimejaa watumishi…
kimejaa dhahabu…
lakini kimefilisika heshima na utukufu!
Trump hakutudhalilisha kwa silaha, bali kwa tabasamu.
Wala hakutushinda kwa jeshi, bali kwa simu ya maongezi!
Basi ni udhalili wa aina gani huu? Na ni Uislamu gani uliobakia ikiwa hatuoni katika tukio hili usaliti wa zama?
Enyi watu…
Hakika adui wa Mwenyezi Mungu, Trump, hakuingia katika ardhi ya Haramain kama mwizi kutoka baharini, wala kama mvamizi kwa ndege, bali aliingia kwa kupitia milango ya miji ya kifalme, katika msafara wa fahari, akipokewa kama "Faatihina" mashujaa washindi!
Akapokelewa kwa heshima kuu, akapewa hazina ili achukue apendacho!
Viongozi walimlaki kwa mfululizo, shingo zikalazwa mbele yake, watu wa mafuta na uamuzi wakamtolea heshima kama kwamba wahyi umeshushwa juu yake kutoka Jabal Radwa!
Na kule Qatar…
Washauri wa Amir na wakubwa wa dola wakamsogelea, si kama kiongozi wa taifa, bali kama “mkombozi” anayepaswa kutiiwa.
Na kule Emirates…
Akapokewa kwa namna ambayo hata wafalme wa zamani hawakuwahi, hadi wanawake wakamchezea densi kama kwamba wao ni warembo wa hadithi za “Alfu Lailah wa Lailah”, lakini kwa mdundo wa tamaduni za Kimarekani, si mashairi ya Kiarabu!
Ngoma yao haikuonyesha ukarimu, bali ilidhihirisha unyenyekevu wa aibu, na Hadhara iliyoporomoka ikikanyagwa na mnyanyasaji huku ikimchekea.
Usiulize kuhusu jizya (kodi ya aibu)!
Hazina zilifunguliwa kwake bila masharti, akapewa kutoka kwa mali ya Waislamu kile ambacho hata mkoloni asingethubutu kuomba kwa jeshi lake.
Ni “jizya ya ridhaa”... haichukuliwi kwa hofu ya upanga, bali kwa tamaa ya kukubalika!
Na uvamizi haukusimama kwa mali tu, bali ukaenda hadi kwenye dini na heshima…
Trump akaketi na mtumishi mpya wa Damascus, mtu aliyewahi kuijaza dunia kwa hotuba kuhusu jihad na ukombozi wa al-Aqsa na waja, lakini sasa anamkalia mbele adui wa Allah kama afisa wa uhusiano wa umma, akisikiliza, anatabasamu, kisha anakubali kuingia kwenye njia ya kusaliti Quds kwa jina la “Tatbii'” Hali ya kawaida na Mayahudi.
Enyi watu…
Kilichotokea si ziara ya kawaida.
Ni tangazo la kifo cha kihadhara mbele ya kamera!
Kama Ummah unampokea muuaji wake kwa kumbatio, linamwekea zulia jekundu, linamweka kwenye viti vya heshima – basi ujue kwamba maadili yamesambaratika, na historia inaandikwa kwa herufi za aibu na fedheha!
Mapokezi haya siyo siasa – ni aibu.
Siyo diplomasia – ni ishara ya kuanguka.
Trump aliingia ardhi ya Waarabu, akawakuta watawala wasio na haiba, majeshi bila aqeeda, wanazuoni wasio na sauti, na wasomi wapiga makofi, huku watu wakiwa kimya kwa unyonge…
isipokuwa wale waliobakia na pumzi ya heshima!
Enyi watu wa nguvu...
Enyi mliohifadhi ndani ya nyoyo zenu ukumbusho wa Uislamu na urithi wa utukufu…
Je, si wakati wa kuinua vichwa kutoka katika aibu hii?
Je, si wakati wa kuvunja minyororo ya unyenyekevu huu?
Je, si wakati wa kutakasa tena ardhi ya Jazira, si kwa kuondoa masanamu ya mawe, bali masanamu ya kibinadamu yanayoitawala leo?
(Enyi mlioamini! Atakayeiacha dini miongoni mwenu, basi Mwenyezi Mungu atakuja na watu wengine, anawapenda na wanampenda, wanyenyekevu kwa Waislamu, wenye nguvu dhidi ya makafiri, wanapigana jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.
(Al-Ma’idah: 54)
– Mundhir Abdullah