
Samson Ernest
May 23, 2025 at 02:27 PM
MTU ANAYEFANYA UOVU KWA MTU ALIYEMTENDEA MEMA AWE NA UHAKIKA AMEKARIBISHA MATATIZO NA MABAYA YOTE
Mit 17:13 SUV
[13] Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake.
Siku za leo sio ajabu kumkuta mtu ambaye alitendewa mema mengi na mtu mwingine, mtu yuleyule alitetendewa mema akageuka na kumfanyia mabaya yule aliyemtendea mema.
Tunaweza kuchukulia kawaida na kuona jambo hili ni la kawaida, ila ukweli lina matokeo mabaya sana kiroho na kimwili.
Mtu anayerudisha mabaya kwa wale waliomtendea mema, awe na uhakika atavuna matatizo na mabaya mengi katika maisha yake.
Mwanzo anaweza asione madhara ya ubaya wake, ila una matokeo ya kushangaza kwa mwenye ubaya huo, atapata shida ambayo anaweza akatafuta suluhisho lake asilipate haraka.
Onyo hili la biblia linaweza kupuuzwa na msomaji asiyetafakari mambo kwa kina, ila mtu anayesoma kwa umakini na kutafakari, hatachukulia kawaida onyo hili.
Tuwe makini katika maisha yetu, kuna watu hawakustahili kurejeshewa mabaya, wapo watu wamejitoa sana kwetu, wametufanya tufike hapo tulipofika, hawatastahili kulipwa mabaya.
Tutende haki, tusimwonee mtu yeyote katika maisha yetu, wale waliotumiwa na Mungu kutufanya tufike mahali tumefika, tuhakikishe tunawapa heshima yao, na tujiepushe kuwatendea mabaya.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma Biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
❤️
🙏
2