
Nukta Habari
June 9, 2025 at 02:24 PM
Kasi ya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mei 2025 umeng’ang’ania katika kiwango cha asilimia 3.2 kama ilivyoripotiwa Aprili, 2025 ikichangiwa zaidi na kupungua kwa kasi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula.
Mfumuko wa bei ni kasi ya ongezeko la bei ya bidhaa na huduma nchini na kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imebainisha kuwa kusalia kwa kasi hiyo ya mfumuko wa bei kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula.
https://nukta.co.tz/mfumuko-wa-bei-tanzania-wanasa-kiwango-cha-aprili-2025