Nukta Habari
Nukta Habari
June 9, 2025 at 02:26 PM
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake, baada ya Bunge la Tanzania kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya NHC wa mwaka 2025 ikiwemo kuipa Bodi ya Wakurugenzi uwezo wa kuwekeza bila kuhitaji idhini ya Waziri wa Ardhi. Marekebisho hayo yanaifanya NHC kuwa na uhuru zaidi katika uwekezaji na utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Mamlaka na Majukumu ya Msajili wa Hazina, Sura ya 370 kuhusu uwekezaji wa mashirika ya umma https://nukta.co.tz/bunge-lapitisha-muswada-wa-sheria-ya-marekebisho-ya-nhc

Comments