Nukta Habari
Nukta Habari
June 9, 2025 at 03:48 PM
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo saba kwa Jeshi la Polisi yanayolenga kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo ikiwemo kuzingatia maadili, kuongeza mapambano dhidi ya dawa za kulevya pamoja na kulinda amani wakati wa uchaguzi. Rais Samia aliyekuwa akihutubia katika sherehe za kuhitimisha mafunzo ya Maofisa na Wakaguzi wa Polisi leo Juni 9, 2025 katika viwanja vya vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Jijini Dar es Salaam amewaambia wahitimu kuwa wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kusimamia viapo vyao. https://nukta.co.tz/maagizo-7-ya-rais-samia-kwa-jeshi-la-polisi

Comments