
Nukta Habari
June 11, 2025 at 03:43 PM
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara katika nchi za Msumbiji na Visiwa vya Komoro ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kihistoria, kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 11, 2025 jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, Rais Samia amepokea mialiko rasmi kutoka kwa Marais wa nchi hizo ili awe mgeni katika maadhimisho muhimu ya kitaifa, yakiwemo ya miaka 50 ya uhuru wa Msumbiji.
https://nukta.co.tz/rais-samia-kufanya-ziara-msumbiji-komoro