
Nukta Habari
June 12, 2025 at 03:29 PM
Deni la Serikali ya Tanzania limeongezeka kwa asilimia 14.9 hadi kufikia Sh107.70 trilioni Aprili 2025 kutokana na kupokelewa kwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Deni hilo limeongezeka kutoka Sh91.71 trilioni ya Machi 2024 au sawa na Sh15.99 trilioni ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
https://nukta.co.tz/deni-la-serikali-ya-tanzania-lafikia-sh107-7-trilioni