Nukta Habari
Nukta Habari
June 12, 2025 at 04:00 PM
Serikali imependekeza kuongeza kodi kwenye bidhaa za pombe zinazoingizwa kutoka nje na sigara za kielektroniki kwa lengo la kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya bidhaa hizo na kuongeza wigo wa kodi. Serikali inalenga kutoza ushuru wa asilimia 30 kwenye vifaa vya sigara za kielektroniki vinavyotambulika kwa HS Code 8543.90.00 na vimiminika vya sigara za kielektroniki vinavyotambulika kwa HS Code 2404.12.00, hatua itakayopeleka maumivu kwa watumiaji wa bidhaa hizo nchini. https://nukta.co.tz/tanzania-yaongeza-kodi-pombe-sigara-za-kielektroniki

Comments