
Nukta Habari
June 12, 2025 at 04:02 PM
Serikali ya Tanzania inapendekeza kuongeza ushuru kwenye bidhaa za gesi na kusamehe baadhi ya kodi ili kuchochea matumizi ya nishati mbadala, kukuza uchumi na kupunguza gharama za maisha.
Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba aliyekuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2025/26 leo Juni 12, 2025 bungeni jijini Dodoma amesema anapendekeza kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwenye gesi asilia kutoka shilingi 0.45 kwa kila futi za ujazo (cubic feet) hadi shilingi 0.55 kwa kila futi za ujazo.
https://nukta.co.tz/serikali-kuongeza-ushuru-bidhaa-za-gesi-asilia-kusamehe-kodi