
Duro Crypto
May 19, 2025 at 03:48 PM
*Crypto vs Hisa: Kuna Tofauti Gani?*
*Cryptocurrency* ni nini?
Cryptocurrency ni pesa za kidigitali ambazo zinatumia teknolojia ya blockchain kuhakikisha miamala ni salama na ya kuaminika. Zinaweza kutumika kama njia ya kulipia au kuhifadhi thamani. Zinapatikana mtandaoni na hazihitaji benki wala taasisi ya kati kuziendesha. Thamani yake inategemea uhitaji na upatikanaji wake sokoni.
*Hisa ni nini?*
Hisa ni umiliki wa sehemu ya kampuni. Ukimiliki hisa, ni kama unamiliki kipande kidogo cha kampuni hiyo. Faida ya kampuni ikiongezeka, unaweza kupata gawio (dividendi). Thamani ya hisa hubadilika kulingana na utendaji wa kampuni na habari mbalimbali kuhusu kampuni hiyo.
*Tofauti Kuu Kati ya Crypto na Hisa*
Ukiwekeza kwenye crypto, hupati umiliki wa kampuni kama ilivyo kwenye hisa.
Crypto haikulipi gawio, ila unaweza kuitumia kupata kipato kwa njia kama staking au yield farming.
Crypto inapatikana saa yoyote, usiku na mchana, kupitia crypto exchanges. Lakini hisa huuzwa kwenye masoko rasmi ya hisa ambayo yana muda maalum wa kufunguliwa.
Crypto ni teknolojia mpya sana ikilinganishwa na hisa ambazo zimekuwepo kwa miongo mingi.
*Je, Niwekeze Wapi, Crypto au Hisa?*
Zote zina faida na changamoto zake. Uamuzi unategemea uvumilivu wako wa hatari (risk tolerance), malengo yako, na muda unaotaka kusubiri kabla ya kuona faida. Wekeza kwa busara na usiweke pesa yote sehemu moja unaweza kuzigawanya kwenye crypto na kwenye hisa.
