Duro Crypto
Duro Crypto
May 31, 2025 at 04:18 PM
*Hatari Zinazoweza Kutokea* *Bei kubadilika sana* Bei ya Bitcoin hupanda na kushuka kwa kasi. Kampuni inaweza kupata hasara kubwa ikiwa bei itashuka sana ghafla. *Usalama* Lazima kampuni ziwe na usalama wa hali ya juu ili kuzuia wizi au kudukuliwa. *Kusahau biashara yao ya msingi.* Kama kampuni itaweka nguvu nyingi kwenye Bitcoin, inaweza kupoteza mwelekeo wa biashara yake ya kawaida. *Mfano wa Kampuni Zenye Akiba ya Bitcoin (Mpaka Mei 2025)* Strategy (MSTR).Hii kampuni ilikuwa inauza programu za kompyuta, lakini sasa imegeuka kuwa kampuni ya kutunza Bitcoin. Inamiliki zaidi ya BTC 576,230, yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 63. Marathon Digital (MARA).Hii ni kampuni ya kuchimba Bitcoin kwa kutumia umeme wa kisasa. Inamiliki BTC 48,100+, zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 5. Riot Platforms (RIOT). Nayo ni kampuni ya kuchimba Bitcoin. Inamiliki zaidi ya BTC 19,200, zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 2. Tesla (TSLA).Kampuni kubwa ya magari. Inamiliki BTC 11,509, zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1. Lakini wao hawajawekeza sana kama wengine. *Mwisho* Kampuni siku hizi zimeanza kubadilika badala ya kuweka pesa tu benki, sasa wanatumia Bitcoin kama njia ya Kuongeza mtaji Kujiandaa na mfumuko wa bei Kuvutia wawekezaji wapya Bitcoin inatoa nafasi mpya kwa kampuni kutunza na kutumia pesa kwa njia ya kisasa zaidi. Kadri crypto inavyozidi kukubalika, njia hii ya kutunza Bitcoin inaweza kuwa mbadala mzuri wa mifumo ya zamani.

Comments