
Duro Crypto
June 5, 2025 at 04:06 AM
*Nifanye Nini Wakati wa Bear Market?*
Kile unachopaswa kufanya wakati soko linaporomoka (bear market) kinategemea na uwezo wako wa kuvumilia hasara na aina ya uwekezaji wako. Kuna njia mbalimbali ambazo watu hutumia kujilinda, ila zinahitaji uvumilivu na mipango mizuri.
*Hapa kuna baadhi ya njia rahisi unazoweza kutumia*
*1. Punguza Uwekezaji*
Kama hujisikii salama wakati bei zinashuka, ni bora kuuza sehemu ya crypto zako na kubaki na pesa taslimu au stablecoins kama USDT.
Kama umewekeza kiasi kikubwa kuliko uwezo wako, ni vizuri kupunguza ili kupunguza hasara.
*2.Kuwa zako Mtulivu tu(HODL)*
Wakati mwingine ni bora kukaa tu na kusubiri soko litulie.
Historia inaonyesha kuwa masoko kama Bitcoin huwa yanapanda tena baada ya muda.
Kama lengo lako ni la muda mrefu (miaka mingi), basi sio lazima kuuza kwa hasara.
*3. Nunua Kidogo Kidogo kwa Muda (DCA)*
Wakati bei zimeshuka sana, wengine hutumia nafasi hiyo kununua kidogo kidogo kwa muda (mfano kila wiki au mwezi).
Hii huitwa DCA unakuwa unanunua bila kujali bei ipo juu au chini.
Kwa njia hii, unakuwa unanunua crypto nyingi wakati bei ni ndogo, na gharama ya jumla inakuwa nafuu zaidi.
4. Pata Faida Wakati Bei Inashuka (Short Selling)
Wale waliobobea kwenye trading wanaweza kupata faida hata wakati bei zinashuka, kwa kutumia mbinu ya short selling.
Pia, unaweza kutumia mbinu ya kujilinda na hasara (hedging). Mfano, ukiwa na BTC 2 kwenye wallet yako, unaweza kuweka nafasi ya kuuza BTC 2 kwenye soko la future, ili ukikosa faida upande mmoja, upande mwingine uifidie.
5. Kununua Wakati Bei Inapanda Kidogo (Counter-Trend)
Wakati mwingine bei hupanda kidogo halafu hushuka tena hii huitwa bear market rally au dead cat bounce.
Wafanyabiashara wengine hujaribu kununua wakati bei inapaa kidogo, halafu huuza mapema kabla bei haijashuka tena.
Hii ni hatari sana, kwa sababu bei inaweza kushuka ghafla na ukapata hasara kubwa.
KUMBUKA: Bear market si mwisho wa dunia. Ni sehemu ya kawaida ya mizunguko ya soko. Muhimu ni kuwa na mpango, kuvumilia na kujifunza zaidi.