
Duro Crypto
June 5, 2025 at 04:14 AM
*Kwa Nini Inaitwa Bear Market?*
Neno "bear market" (soko la dubu) linatokana na mfano wa dubu anapopiga kwa makucha yake kuelekea chini, kuashiria jinsi bei zinavyoshuka kwa kasi.
Kwa upande mwingine, "bull market" (soko la fahali) linatokana na fahali anayepiga kwa pembe zake kuelekea juu, kuashiria bei zinazopanda.
Haya maneno yamekuwa yakitumika tangu karne ya 19.
Kuna maelezo yanayosema jina “bear” lilitokana na watu waliokuwa wanauza ngozi za dubu hata kabla hawajazipata, mfano wa leo ni kama short selling.
*Hitimisho*
Bear market mara nyingi husababishwa na matatizo ya kiuchumi, kisiasa au hali ya wasiwasi miongoni mwa wawekezaji. Ingawa kipindi hiki huwa kigumu, ni sehemu ya kawaida ya mzunguko wa masoko ya fedha.
Kwa kuwa na nidhamu na mipango mizuri, mtu anaweza kujilinda dhidi ya hasara, au hata kupata faida wakati bei zinaporomoka.
Wakati wa bear market
Wengine huamua kuendelea kushikilia (HODL) uwekezaji wao bila kuuza.
Wengine hupunguza hatari kwa kuhifadhi pesa taslimu, stablecoins au kuhamia kwenye mali zisizo na mabadiliko makubwa kama bonds.
Mbinu ya kununua kidogo kidogo kwa muda mrefu (DCA) pia hupendwa na wengi.
Kwa waliobobea, short selling na counter-trend trading ni mbinu hatari lakini zinaweza kutoa faida kama zitafanywa kwa uangalifu mkubwa.