
Duro Crypto
June 11, 2025 at 05:44 PM
1. *Korea Kusini kuhalalisha stablecoins* .
Chama tawala nchini Korea Kusini kimewasilisha muswada mpya wa sheria (Digital Asset Basic Act) utakaoruhusu kampuni za ndani zenye mtaji kuanzia TZS billioni 1.2 kuanzisha stablecoins. Lengo ni kuzuia pesa kutoroshwa nje ya nchi na kukuza sekta ya teknolojia ya fedha.
*2 BlackRock imevunja rekodi ya dunia na Bitcoin ETF yao (IBIT)*
Mfuko wa IBIT wa kampuni ya BlackRock umefikia thamani ya TZS trilioni 187 (USD bilioni 70) kwa haraka zaidi kuliko ETF yoyote duniani, ishara kuwa wawekezaji wakubwa sasa wanauchukulia Bitcoin kama mali rasmi ya uwekezaji wa muda mrefu.
3. *Bunge la Marekani lapitisha hatua ya kwanza ya sheria ya Crypto (CLARITY Act)*
Kamati mbili kubwa za Bunge la Marekani zimepitisha muswada wa sheria mpya ya crypto. Sheria hii inalenga kutoa tafsiri ya wazi juu ya ni taasisi gani itasimamia crypto kama ni SEC (kama hisa) au CFTC (kama bidhaa).
*4 .Visa & Chainlink waonyesha mafanikio ya miamala ya CBDC kati ya nchi*
Visa kwa kushirikiana na Chainlink wamefanya jaribio la mafanikio la kubadilisha fedha za kidigitali kati ya Hong Kong (e-HKD) na Australia (A$DC), bila kutumia benki ya kati au taasisi ya kati. Teknolojia ya blockchain inaonesha thamani katika miamala ya kimataifa.
*5 Mmiliki wa kampuni ya crypto kutoka Urusi akamatwa kwa kutakatisha TZS trilioni 1.3*
Mwanaume aitwaye Iurii Gugnin a.k.a George Goognin amekamatwa Marekani kwa madai ya kutumia kampuni yake ya crypto kutakatisha mabilioni ya pesa kwa niaba ya mashirika ya Kirusi yaliyowekewa vikwazo. Anakabiliwa na mashtaka 22.

🤝
1