Duro Crypto
Duro Crypto
June 11, 2025 at 07:33 PM
*NFT ni Nini?* Hebu fikiria hivi: una picha ya kipekee sana, au tiketi ya tamasha kubwa, au hata mchoro mzuri wa sanaa, lakini si kitu cha kawaida cha kushikika, ni cha kidigitali tu. Sasa, ukiwa na hiyo picha au tiketi kwenye simu yako au kompyuta, mtu mwingine si anaweza kuikopi kirahisi, si ndiyo? Lakini kwa kutumia NFT, hiyo picha au tiketi inakuwa yako pekee, hakuna mwingine atakayekuwa na haki ya kuimiliki au kuisambaza kama yake. NFT ni mali ya kidijitali inayothibitisha kuwa kitu fulani cha mtandaoni ni chako halali. Hii mali huhifadhiwa kwenye mfumo salama unaoitwa blockchain, ambao unafanya kazi kama daftari lisilofutika, kila mtu anaweza kuona nani anamiliki kitu fulani.
Image from Duro Crypto: *NFT ni Nini?*   Hebu fikiria hivi: una picha ya kipekee sana, au tike...

Comments