
Duro Crypto
June 11, 2025 at 07:39 PM
*NFT Inatumiwaje?*
NFT inaweza kuwa kitu chochote cha kidijitali:
Picha ya sanaa
Muziki
Tiketi ya kuingia kwenye show
Kiwanja kwenye ulimwengu wa mtandaoni (metaverse)
Hata mavazi ya kuvaa kwenye michezo ya mtandaoni!
Na yote hayo, ukiwa na NFT yake, unakuwa mmiliki halali. Ni kama cheti chako cha umiliki, lakini cha mtandaoni.
*Wabunifu Wananufaikaje?*
Zamani msanii alitegemea kuuza picha zake kupitia maonyesho au madalali.
Lakini sasa, kwa kutumia NFT, msanii anaweza kuuza kazi yake moja kwa moja mtandaoni, na kila anayenunua anaweza kuithibitisha kuwa ni ya kwake.
Na pia msanii anaweza kupata faida kila mara kazi yake inapouzwa tena.Kazi yake inazidi kumlipa hata baada ya kuuza. Hii imeleta mapinduzi kwa wasanii, wabunifu, na hata wanamuziki.
*NFT Staking - Njia ya Kupata Faida*
Sasa hivi kuna njia nyingine pia ya kunufaika na NFT:
Unaweza kuiweka kama dhamana (stake), halafu upate zawadi au riba kila mwezi, bila kuuza hiyo NFT.
Ni kama vile unavyoweka pesa benki upate riba, lakini safari hii unaweka NFT kwenye jukwaa maalum la kifedha (DeFi).
*Tiketi za NFT - Suluhisho la Tiketi Feki*
Waandaaji wa matamasha au mechi wanaweza kutoa tiketi kwa mfumo wa NFT.
Tiketi hizi ni salama, hazighushiwi, na mtu anaweza kuziuza au kumpa mwingine bila kutumia wakala.
Cha kuvutia zaidi, tiketi hizi zinaweza kuja na faida za ziada kama:
Kuingia eneo la VIP
Kupata zawadi maalum
Kuona maudhui ya kipekee mtandaoni