Duro Crypto
Duro Crypto
June 11, 2025 at 07:51 PM
*Mifano Maarufu ya NFT* *CryptoPunks* Hii ni picha yenye picha 10,000 tofauti zilizotengenezwa kwa mfumo wa kompyuta. Kila picha ni ya kipekee, kama avatar za watu wa pixel. Baadhi ya watu mashuhuri walizitumia kama picha zao za profile kwenye mitandao ya kijamii. Bored Ape Yacht Club (BAYC) Hizi ni picha za nyani zenye muonekano wa katuni, kila moja ikiwa tofauti. Ukimiliki moja, unapata mialiko ya matukio maalum, na maeneo ya kipekee mtandaoni. Ni kama klabu ya watu maalum, lakini ya kidigitali. *Decentraland* Hapa watu hununua ardhi, majumba na vitu mbalimbali kwenye ulimwengu wa mtandaoni. Unamiliki mali za mtandaoni kwa kutumia NFT, yaani hata maisha ya kidigitali sasa yanahitaji umiliki!

Comments