Duro Crypto
Duro Crypto
June 11, 2025 at 08:05 PM
*Makosa ya Kawaida ya Watu Kuhusu NFT* *Usidanganyike* 1. “NFT ni salama kabisa, hakuna shida!” Ni kweli, NFT zinatumia blockchain, teknolojia ambayo ni salama sana. Lakini hiyo haimaanishi kuwa hakuna hatari kabisa! - Kuna matapeli wa link feki (phishing) - Unaweza kununua NFT ya bandia, ambayo haijaidhinishwa na mmiliki halali - Thamani ya NFT inaweza kushuka ghafla bila kutarajia 👉 Kwa hiyo, kuwa makini! Si kila kitu kwenye blockchain ni salama 100% 2. “NFT ni sawa tu na pesa za mtandaoni (crypto)” Hapana kabisa! Hivi ni vitu viwili tofauti Cryptocurrency (kama Bitcoin) ni kama pesa unaweza kubadilishana bitcoin moja na nyingine kwa thamani ile ile. NFT ni kitu cha kipekee, mfano wa mchoro au kitu maalum. Huwezi kubadilisha NFT moja kwa nyingine kwa thamani sawa moja kwa moja. Kwa kifupi Crypto = pesa NFT = mali ya kipekee (haifanani na nyingine)

Comments