
Jimbo Katoliki Kigoma
June 7, 2025 at 10:28 AM
Hayati Baba Mtakatifu Francisko, kabla ya kifo chake, alimtunuku heshima ya Monsinyori (Monsignor) Pd. Metteo Linus Ntamaboko.
Hivyo Padre Ntamaboko ambaye mpaka sasa ni mwalimu na mlezi wa seminari ndogo ya Mtakatifu Yosefu Iterambogo, na kwa namna pekee akiadhimisha mwaka huu 2025 Jubilei ya Miaka 50 ya ukasisi anatambulika sasa kwa heshima hiyo kubwa aliyotunukiwa na hivyo anaitwa Monsinyori (Mons) Matteo Linus Ntamaboko.

🙏
❤️
👏
🥂
🥳
6