
Jimbo Katoliki Kigoma
490 subscribers
About Jimbo Katoliki Kigoma
Habari na Matukio ya uinjilishaji kutoka Kanisa Katoliki, Jimbo la Kigoma, Tz.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

https://youtu.be/sFurYE7qGqY?si=2loP3mFnUylHxKQM

Mhashamu Joseph Roman Mlola ALCP/OSS Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Ametoa kibali maalumu cha ubatizo wa watoto walio chini ya umri wa miaka 7. Kibali hicho amekitoa kupitia barua ya kichungaji kwa Padre,watawa na waamini wote jimboni Kigoma yenye Kichwa cha Habari *ENENDENI DUNIANI KOTE* iliyotolewa June 3,2025 katika sherehe za kumbukumbu ya watakatifu Mashahidi wa Uganda. Katika barua hiyo ameeleza kuwa katika mwaka huu wa jubilei ya miaka 2025 ya Kristo wazazi na walezi watumie neema hiyo jubilei kuwa batiza watoto ambao hawajapata sakramenti hiyo muhimu ya kuwaingiza katika sakramenti zote za Ukristo. Amesema imebainika kuwa kuna watoto wengi katika familia ambao hawajapata ubatizo kutokana na Sababu mbalimbali ziliwemo za wazazi kutokuwa na huduma za sakramenti. Hivyo ubatizo huo utatolewa kwa watoto ambao wazazi wao hawana huduma za sakramenti katika Kanisa. Katika barua hiyo Mhashamu Joseph Mlola, amewataka wale wote watakao batizisha watoto kufuata mafundisho maalumu kwa kipindi kwa miezi 3 mfululizo ikiwa ni wao pamoja na wasimamizi wao ili kuwaimarisha zaidi Kiroho. Sambamba na hayo katika barua yake ya kichungaji amehizima kuwa ubatizo huo utatolewa kufauata taratibu za kanisa na zile za Parokia kadri ya mashariti na melekezo msingi ya Parokia.


SEAT OF WISDOM ENGLISH MEDIUM SCHOOL, KASULU

Hayati Baba Mtakatifu Francisko, kabla ya kifo chake, alimtunuku heshima ya Monsinyori (Monsignor) Pd. Metteo Linus Ntamaboko. Hivyo Padre Ntamaboko ambaye mpaka sasa ni mwalimu na mlezi wa seminari ndogo ya Mtakatifu Yosefu Iterambogo, na kwa namna pekee akiadhimisha mwaka huu 2025 Jubilei ya Miaka 50 ya ukasisi anatambulika sasa kwa heshima hiyo kubwa aliyotunukiwa na hivyo anaitwa Monsinyori (Mons) Matteo Linus Ntamaboko.
