
Jimbo Katoliki Kigoma
June 7, 2025 at 10:40 AM
Mhashamu Joseph Roman Mlola ALCP/OSS Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma
Ametoa kibali maalumu cha ubatizo wa watoto walio chini ya umri wa miaka 7.
Kibali hicho amekitoa kupitia barua ya kichungaji kwa Padre,watawa na waamini wote jimboni Kigoma yenye Kichwa cha Habari *ENENDENI DUNIANI KOTE* iliyotolewa June 3,2025 katika sherehe za kumbukumbu ya watakatifu Mashahidi wa Uganda.
Katika barua hiyo ameeleza kuwa katika mwaka huu wa jubilei ya miaka 2025 ya Kristo wazazi na walezi watumie neema hiyo jubilei kuwa batiza watoto ambao hawajapata sakramenti hiyo muhimu ya kuwaingiza katika sakramenti zote za Ukristo.
Amesema imebainika kuwa kuna watoto wengi katika familia ambao hawajapata ubatizo kutokana na Sababu mbalimbali ziliwemo za wazazi kutokuwa na huduma za sakramenti.
Hivyo ubatizo huo utatolewa kwa watoto ambao wazazi wao hawana huduma za sakramenti katika Kanisa.
Katika barua hiyo Mhashamu Joseph Mlola, amewataka wale wote watakao batizisha watoto kufuata mafundisho maalumu kwa kipindi kwa miezi 3 mfululizo ikiwa ni wao pamoja na wasimamizi wao ili kuwaimarisha zaidi Kiroho.
Sambamba na hayo katika barua yake ya kichungaji amehizima kuwa ubatizo huo utatolewa kufauata taratibu za kanisa na zile za Parokia kadri ya mashariti na melekezo msingi ya Parokia.

🙏
👍
5