Dr Nature
Dr Nature
May 19, 2025 at 06:05 PM
Suppliments: Tiba ya Haraka au Sumu ya Polepole?” Katika dunia ya sasa matumizi ya virutubisho vya lishe (supplements) yamekuwa jambo la kawaida. Kuanzia vidonge vya vitamini, protini powder, mafuta ya omega-3 nk na madini kama zinki na chuma nk. Lakini kwenye wengi pana mengi.. haya ni mambo ambayo unatakiwa kuwa nayo akilini.. 1. VIRUTUBISHO SI DAWA YA MIUJIZA Lishe ambayo kwa sehemu kubwa inatokana na mimea katika uasili wake (whole food plant-based diet) ndiyo njia sahihi ya kupata virutubisho vyote muhimu. Kulingana na tafiti nyingi virutubisho vingi havijathibitishwa kuwa na manufaa kwa watu. Hata mamlaka zinazodhibiti ubora wake mara nyingi hutegemea maabara za viwanda husika zitoe ubora wake. Kwa mfano: • Vitamini E na beta-carotene supplements zimehusishwa na ongezeko la hatari ya kansa. • Calcium supplements zimeonekana kuongeza hatari ya mshtuko wa moyo badala ya kusaidia mifupa kama inavyodhaniwa. 2. CHANGAMOTO ZA KIAFYA ZINAZOTOKANA NA SUPPLEMENTS • Zinaweza kusababisha Overdose: Mfano vitamini zinazoyeyuka kwenye mafuta kama A, D, E, na K zinawezakusababisha sumu (toxicity) zikitumika kwa wingi. • Kupingana na Dawa: Virutubisho vinaweza kuingiliana na dawa za hospitali, na kusababisha madhara au kupunguza ufanisi wa dawa. • Uthibitisho Hafifu wa Ufanisi: Tafiti nyingi zinazoteteta virutubisho hufadhiliwa na makampuni ya kutengeneza bidhaa hizo, hivyo kushusha ushahidi wa kisayansi. • Uhaba wa Udhibiti (Regulation): Viwango vya ubora na usalama wa virutubisho havidhibitiwi kwa ukali kama dawa, hivyo bidhaa nyingi zinaweza kuwa na viambato visivyo sahihi au hatari. 3. LISHE ASILIA NDIO SULUHISHO Ni rahisi kupata virutubisho unavyotaka kutoka kwenye chakula. Mfano; • Badala ya vidonge vya kuongeza madini ya chuma → kula dengu, mbegu ya parachichi, spinach, na mbegu za maboga. • Badala ya omega-3 capsules → kula mbegu za chia, flaxseed, na walnuts. • Badala ya protini powders → kula maharage, kunde, mbegu na karanga. 4. HATA HIVYO SIO “BLACK AND WHITE” Nilichokisema ni taarifa ambazo zinakusaidia kuchukua tahadhari. Sio kila kinachoitwa ni kirutubisho kinafaa mwili wako • Vingine vinafaida zinazoweza kukuvusha katika hali Fulani ya kiafya kirahisi na kujazia ambapo hujaweza kufanya kwa chakula • vingine havina faida yoyote na hivyo uapoteza pesa yako, • vingine vina madhara usipotumia kwa usahihi • Vingine ni sumu kabisa haifai kugusa Unahitaji Kwenda pole kwa uangalifu kama unavyoziendea dawa. Ushawishi wa kampuni au muuzaji usikuchukue bila kujiridhisha usalama na ufanisi wake.
❤️ 🙏 7

Comments