
Dr Nature
June 10, 2025 at 05:02 AM
Nikiwa Mawenzi Hospital 2022 usiku huo nilikuwa mergency akaletwa mwanamke mmoja miaka 36 amelegea kiasi kwamba hata kupumua anapumua kwa shida..
Baada ya kumpa hduma ya kwanza akanieleza kuwa ametumia dawa ya kupunguza uzito ameharisha na kutapika. Na bahati mbaya hadi analegea mume wake alikuwa mbali akakosa msaada mapema.
Usitumie dawa ya kuharisha kupunguza uzito au kitambi. Mafuta hayakai kwenye utumbo yapo kwenye seli za mafuta.
Ongeza metabolisim ili yachomwe sio kuharisha au kutapika.
Ukiharisha na kutapika unapoteza maji na madini 'electrolytes' ni HATARI sana, unaweza kupotea siku sio zako

🙏
👍
4