
SITTA SPORTS ARENA
June 12, 2025 at 04:35 PM
*IBRAHIMOVIC AJA KUTALII TANZANIA ⚽*
Nyota wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic yupo Nchini Tanzania ambapo ame‘post’ picha akiwa eneo la Kogatende kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania eneo ambalo ni kitovu cha uhamaji wa wanyama maelfu wanaovuka Mto Mara.
Zlatan (43) raia wa Sweden ambaye amewahi pia kuichezea Ajax, PSG, AC Milan na Barcelona ambaye kwa sasa ni sehemu ya washauri wa klabu ya AC Milan yupo Tanzania kwa ajili ya mapumziko ya mwisho ya msimu.
SITTA SPORTS UPDATES ⚽
