MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
May 23, 2025 at 04:11 PM
*MUKHTASAR WA IBADA YA HIJJA NA 'UMRAH:* ________________ ●Maandalizi ya safari ya Hijja No. 0️⃣4️⃣ 5. *Achague mali ya halali:* chumo lake liwe la halali na kuihudumia familia yake kwalo kwa kiasi ambacho Allaah amemkunjulia. Asiwe ni mwenye azma ya kwenda kufanya Hijja au 'Umra lakini chumo lake na matumizi yake ni katika yale yasiyomridhisha Allaah. 6. *Kuusia kunako kumcha Allaah _subhaanahu wata'alaa _ kwa siri na kwa dhahiri.* Muislamu yampasa aiusie nafsi yake na watu wake daima kwa kumcha Allaah na kufanya maamrisho na kuachana na makatazo katika maasi, hasa hasa wewe uliyeikusudia ibada hii. Kwani Taqwa hiyo ndiyo zawadi bora zaidi. 7. *Uwajibu wa kufahamu matendo ya Hijja na 'Umrah:* mtu anatakiwa ajifunze ibada hii kabla ya kuitekeleza ili ajue usahihi wa utekelezwaji wake kama alivyoelekeza Mtume _swalla llaahu 'alayhi wasallama_ Na ikiwa kuna jambo linamtatiza au halifahamu afanye pupa ya kuwauliza wanachuoni. ...... inaendelea
Image from MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚: *MUKHTASAR WA IBADA YA HIJJA NA 'UMRAH:*   ________________     ●Maand...

Comments