MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
May 23, 2025 at 04:19 PM
8. Hii ni maalum kwa wenye kuwapeleka watu Hijja na 'Umra: *wasionekane vituko zaidi ya wale mahujaji wao:* Hawa viongozi wa taasisi wawe kama mfuaji/msafishaji wa nguo au chombo - mikono yake isafike zaidi. Isiwe Hajj (aliyekwenda Hijja) tena ndio kwanza awamu ya kwanza akawa na uafadhali kwenye utekelezaji wa ibada kuliko yeye, au akageuka kituko kwenye ibada hizo - ima kwa kupuuzia au kuleta mchezo na masihara kwa vile kwake limekuwa jambo la mazoea. Tubadilikeni waja wa Allaah - hasa tunapokuwepo kwenye ibada hizo na pale tunaporudi tuwe mifano mizuri kwa wengine tusiangalie maslahi yetu tu, bali tuangalie zaidi maslahi ya ibada hii. 9. *Tumuombe Allaah tawfiiq:* Allaah atuwafikishe kuweza kuitekeleza ibada hii - huku tukiamini kuwa sio mali zetu wala afya zetu kuweza kuitekeleza ibada hii bali ni kwa Tawfiiq yake Allaah - hivyo mtu asifanye mchezo katika ibada yake hii. Pia tuwaombee wale ambao Allaah hajawawafikisha kuitekeleza hii ibada - awatie nguvu nao waitekeleza kwa kutafuta radhi zake Allaah subhaana. Baaraka llaahu fiikum

Comments