MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
May 23, 2025 at 09:49 PM
SHAIRI: SEMA NAYE Mtunzi: Tulaybu 1.Naukunjua mkeka, njoo tushauriane Dada yangu pia kaka, nasaha tuambiane Kamwe tusifuge taka, vema tunasihiane Mapema useme naye, singoje muda upite 2.Sema na wako mtoto, mapema angali chini Ni baridi au joto, mfunze awe makini Awe Kurwa au Doto, mpe maneno laini Mapema useme naye, singoje muda upite 3.Mpe elimu kijana, elimu ya maadili Ya leo sio ya jana, azitulize akili Sema bila kuyabana, yasimzonge maswali Mapema useme naye, singoje muda upite 4.Watoto lao hitaji, wayafikie malengo Hivyo kwenye ukuaji, usiwaachie pengo Wasiwe wazururaji, maisha ya songombingo Mapema useme naye, singoje muda upite 5.Hali imeshachafuka, kwa wakike na kiume Watoto wahitajika, maadili wayasome Sio usiku kuruka, mithili ya paka chume Mpema useme naye, singoje muda upite 6.Mjengee marafiki, wema wasio waovu Sio wale wanafiki, mwanao mpe makavu Muonye kama hataki, kwa upole utulivu Mapema useme naye, singoje muda upite 7.Ukae naye karibu, mfanye wako swahiba Umzoeshe vitabu, hwena akaleta toba Atazijua adhabu, maovu akiyabeba Mapema useme naye, singoje muda upite _____________________ Sat, 24 May 2025 Tulaybu ✍️ 0714388284
Image from MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚: SHAIRI: SEMA NAYE Mtunzi: Tulaybu  1.Naukunjua mkeka, njoo tushauriane...
👍 1

Comments