
MEFTAHUL 'ULUUM 📚🔑📚
May 26, 2025 at 07:43 PM
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته
*NDUGU ZANGU:*
Umma umeghaflika sana na masiku ya kheri na ibada zake.
Badala yake umma umegubikwa na mambo ya michezo na pumbao.
Hakuna nafsi inajua lini na nini kinafanyika katika masiku haya bora, si kike si kiume, si mdogo wala mkubwa, bali mpaka wenye kujinasibu na dini wakiwemo waalimu na maimamu na ambao hawakosekani kwenye misikiti lakini mtihani mkubwa ni kusikia mijadala ya michezo misikitini na watu wa misikiti.
Huu ni msiba ndugu zangu, majumba yamejaa ushetani hakuna anayekemea.
*HAYA YANAYOINGIA NI MASIKU KUMI BORA:*
Masiku ambayo amali ya mtu katika masiku haya ni bora mno na yenye fadhila na ujira mkubwa haya ni *MASIKU KUMI YA DHULHIJJA*
Tuitumieni fursa hii, kwa kufanya matendo mazuri.
Allaah aliowakunjulia wakaenda Hijja na ambao watachinja wanyama na amali nyengine hata zile unazoziona no ndogo usidharau chochote kwani hwenda kikawa kina ujira mkubwa sana.
Baaraka llaahu fiikum