JamiiForums

JamiiForums

716.2K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
June 13, 2025 at 04:36 PM
DODOMA: Akisoma majibu ya barua yao ya Rufaa yaliyotumwa kwao Juni 6, 2025 kutoka Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Wakili Peter Kibatala ametoa maelezo akisema barua iliyotumika kulifungia Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Kanisa la Ufufuo na Uzima haitambuliki na Mamlaka iliyotajwa kulifungia Ameyazungumza hayo leo Juni 13, 2025 baada ya kutoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo, ambapo upande wa Kanisa ukiwakilishwa na Wakili Kibatala unaiomba Mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini Soma https://jamii.app/KanisaLaGwajima
👍 😢 🙏 ❤️ 😁 😂 😮 19

Comments